Description
Biblia: Kitabu cha Ufunuo na Mwongozo
Biblia, zaidi ya kitabu, ni ufunuo wa Mungu kwa wanadamu, iliyoandikwa kwa upendo na hekima. Ni kitabu kilicho hai, kilichovuviwa na Roho Mtakatifu, na chenye maneno ya mwandishi mkuu. Ujumbe wake ni takatifu, maandiko yake ni matakatifu, na lengo lake kubwa ni kutuongoza kwenye utakatifu.
Historia na Uandishi wa Biblia
Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40 kwa muda wa zaidi ya miaka 1500 (kuanzia 1400 K.K. hadi 100 B.K.). Iliandikwa na vizazi zaidi ya 40, katika mazingira, nyakati, na mabara tofauti (Asia, Ulaya, na Afrika), na katika lugha tatu (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani). Karibu Agano la Kale lote liliandikwa kwa Kiebrania, isipokuwa sehemu chache za kitabu cha Danieli ambazo ziliandikwa kwa Kiaramu. Agano Jipya liliandikwa kwa Kigiriki.
Upatikanaji na Umuhimu wa Biblia Leo
Kufikia mwanzoni mwa mwaka 2007, Biblia nzima ilikuwa imekwisha tafsiriwa katika lugha 429. Agano Jipya au Agano la Kale pekee vilikuwa vimekwisha tafsiriwa katika lugha 1144. Biblia nzima ilikuwa tayari imekwisha tafsiriwa katika lugha za Afrika mia moja sitini. Biblia ilikuwa kitabu cha kwanza kuchapishwa na mashine mwaka 1455 na Johann Gutenberg.
Vitabu vingine huchakaa, lakini Biblia hupita vizazi vyote. Vitabu vingine lazima vibadilishwe ili kuendana na wakati, lakini Biblia hupendwa na wazee kwa vijana. Vitabu vingi vinalenga sehemu ndogo ya watu na huvutia watu wa lugha fulani tu, lakini Biblia ni tofauti. Ina vitabu 66: 39 katika Agano la Kale na 27 katika Agano Jipya. Biblia ina sura 1,189 (929 katika Agano la Kale na 260 katika Agano Jipya). Katika Biblia ya Kiswahili, kuna mistari 31,102 (23,145 katika Agano la Kale na 7,957 katika Agano Jipya). Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2 Petro 1:21). Biblia ni mwongozo wa maisha na chanzo cha hekima kwa wote.
Reviews
There are no reviews yet.