Description
Mwanzo wa Taifa la Israeli: Utangulizi
Safari ya taifa la Israeli inaanza na mtu mmoja muhimu, Ibrahimu, anayeheshimiwa sana katika Biblia, Torati, na Quran. Kinachovutia kuhusu Ibrahimu ni kwamba dini kuu tatu za ulimwengu—Uislamu, Ukristo, na Uyahudi—zote zinamtambua na kumheshimu kama baba wa imani yao.
Nafasi ya Ibrahimu Katika Imani Tofauti
Wakristo: Wanamwona Ibrahimu kama baba wa imani, mtu ambaye alitabiriwa kuwa uzao wake ungemleta Mwokozi, Yesu Kristo. Ibrahimu ni mfano wa kuigwa linapokuja suala la imani. Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu, Wakristo wanamwamini Yesu Kristo.
Waislamu: Wanamheshimu Ibrahimu kama mtu mwenye imani thabiti kwa Mola. Hata hivyo, Waislamu hawaamini kwamba Ibrahimu alikuwa Myahudi au Mkristo. Pia, hawakubali kwamba mtoto wa Ibrahimu aliyekusudiwa kutolewa kafara alikuwa Isaka. Ingawa hawasemi waziwazi, wanaamini aliyekusudiwa kutolewa kafara alikuwa Ishmaeli, mtoto wa Ibrahimu na kijakazi wake, Hajiri. Madai haya yanapingana na yale yaliyoandikwa katika Biblia.
Wayahudi: Wanamheshimu sana Ibrahimu. Wanamwona kama baba yao, mwanzilishi wa taifa la Israeli, na mtu aliyemcha Mungu kwa imani yake. Madai haya hayapingiki, kwani yameelezewa wazi katika Biblia—Torati, Zaburi, Manabii, na Agano Jipya.
Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Mwanzo wa Israeli
Mungu alimwambia Ibrahimu aondoke na mke wake kutoka kwa ndugu zake na familia yake, akiahidi kumfanya kuwa taifa kubwa. Mungu aliamua kwamba kupitia Ibrahimu, atazaa taifa litakalokuwa lake kwa kumwamini. Unaweza kusoma habari hii kwa undani zaidi katika kitabu cha Mwanzo 12.
Reviews
There are no reviews yet.