Description
Mungu: Chanzo cha Mission
Bwana anajifunua kama Mungu aliyetafuta kilicho potea. Sisi watu wake, tunapaswa kumfuata! (Fil 2:5). Tazama jinsi alivyowatafuta watu:
– Yeye mwenyewe alimtafuta Adamu (Mwa 3:9)
– Alimwita Ibrahimu (Mwa 12)
– Alimtuma Yusufu (Mwa 45:4-8)
– Musa aliitwa na kutumwa (Kut 3:7-10)
– Aliwatuma manabii (Yer 7:25)
– Alimtuma Yona kwa mataifa (Ninawi)
– Zaburi zinataja mataifa (ulimwengu wote) mara 140, ingawa ni kitabu cha nyimbo cha Uyahudi (Zab 117)
– Alimtuma Yesu Kristo kama Mwokozi wa ulimwengu (Yohane 3:16, 4:42, Fil 2:7-8, 2 Kor 8:9)
– Roho Mtakatifu alitumwa duniani (Mdo 2:33)
– Yesu alituma mitume wake (Mt 28:18-20, Yoh 20:21)
Daraka la Kanisa katika Mission
Kanisa limepewa daraka la kuendeleza utume (Mdo 13:1-4, Rom 10:11-17). Mfano: Kanisa la Antiokia (Mdo 21:23).
Wito kwa Wakristo
Sisi kama watu wa Mungu, tunapaswa kuona moyo wa mission ndani ya Mungu, ndani ya Yesu Kristo, na ndani ya Roho Mtakatifu. Daraka letu ni kuwahamasisha Wakristo waweze kushiriki kikamilifu katika mission, wakikubali kuvuka mipaka, kuwa tayari kujitoa kimwili na kiroho, hata mali zetu, kwa kueneza Injili mahali ambapo bado haijafika.
Reviews
There are no reviews yet.